Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Infantinno yazua utata Kombe la Dunia la Wanawake

Infantino Gianni FIFA Rais wa FIFA Gianni Infantino

Sat, 19 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa FIFA Gianni Infantino amekosolewa vikali kwa kusema kuwa wacheza soka wakike wanatakiwa kuchagua vita sahihi katika vita yao ya kutaka kulipwa sawa na wanaume katika Kombe la Dunia.

Kuelekea fainali za Kombe la Dunia la Wanawake, Infantino ametoa hotuba ambayo imeonekana ina utata “Nasema kwa Wanawake wote, na mnajua nina mabinti wanne, hivyo nami nina wanawake kiasi nyumbani, nawaambia wanawake wote mnayo nguvu ya kubadilika”

”Chagueni vita sahihi, chagueni mapambano sahihi, mnayo nguvu ya kutushawishi sisi wanaume kile tunachotakiwa kufanya na tusichotakiwa kufanya. Fanyeni tu”

”Kwetu wanaume na kwa FIFA mtakuta milango iko wazi, sukumeni milango, iko wazi”.

Kauli hizo zimezua gumzo na kuelekeweka kama Infantino anamaanisha ni jukumu la wanawake kuchukua hatua sahihi ili wapate usawa.

Tuzo ya fedha katika Kombe la Dunia la Wanawake 2023 imeongezeka na kuwa dola za Kimarekani Milioni 110, ambayo ni mara tatu ya kiasi kilichotolewa kwa Kombe la Dunia la mwaka 2019.

Hata hivyo kiasi hicho bado ni kidogo ukilinganisha na kiasi kilichotolewa kwa Kombe la Dunia la Wanaume 2022 Qatar, ambacho kilikuwa ni dola za kimarekani 440.

Fainali za Kombe la Dunia la Wanawake zitafanyika Jumapili Agosti 20 huko Sydney, Australia ambapo timu ya Taifa ya Hispania itachuana na timu ya Taifa ya England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live