Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Aziz Ki baada ya kutua kambini

AZIZ KI AVIC YANGA D Kauli ya Aziz Ki baada ya kutua kambini

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephane Aziz KI ameripoti kambini jana na kuanza mazoezi moja kwa moja na kikosi kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AL Hilal ya Sudan.

KI alichelewa kujiunga kambini kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Uviko 19 aliyoipata akiwa na Timu yake ya Taifa ya Burkina Faso.

Akizungumza baada ya kutua kambini Avic Town, Kigamboni, Aziz Ki ametoa shukrani zake kwa Uongozi wa Yanga SC kwa kumpa ushirikiano mkubwa alipokuwa Morocco na kuhakikisha amerejea salama kambini.

“Nimerejea salama. Nawashukuru viongozi wa Yanga kwa kuwa pamoja na mimi wakati ambao nilikumbwa na kadhia hiyo. Naendelea vizuri, sina shida yoyote,” alisema Aziz Ki.

Kuelekea mchezo wa Al Hilal, Aziz amewaomba mashabiki wa Yanga kwenda kwa wingi uwanjani na kuishangilia timu yao akiamini hiyo itakuwa chachu kubwa kwa wachezaji kujituma zaidi.

“Nina matumaini makubwa tutafanya vizuri, tunachohitaji ni mashabiki kutuunga mkono kwa kufika uwanjani. Uwepo wao utakuwa chachu kubwa kwetu kuongeza bidii,” aliongeza Aziz.

Aziz Ki amekuwa kwenye kiwango kizuri akiwa tayari ameshafunga magoli mawili mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live