Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Azam FC kuhusu Fei Toto

Azam Fei Kauli ya Azam FC kuhusu Fei Toto

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Azam FC kuhusishwa na dili la kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe, ameibuka na kuvunja ukimya.

Fei Toto ambaye amekuwa ndani ya Yanga tangu mwaka 2018, imeripotiwa kwamba ameandika barua ya kuvunja mkataba wake uliobaki mwaka mmoja na nusu, huku akihusishwa kupata dili la kwenda Azam.

Kiungo huyo mwenye mabao sita katika Ligi Kuu Bara msimu huu, juzi hakucheza mechi ya ligi hiyo dhidi ya Azam wakati Yanga ikishinda 2-3 Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza, Ibwe alisema moja kwa moja hawezi kuzungumzia usajili wa Fei Toto kutua kikosini kwao kipindi hiki, lakini muda ukifika, kila kitu kitafahamika.

“Kwa sasa siwezi kuzungumzia suala la Feisal, japokuwa mengi yamesemwa kuwa tunamsajili mchezaji huyo na tumehusika kwa namna moja au nyingine kuondoka kwake katika Klabu ya Yanga.

“Muda ndiyo utakaoongea, baada ya muda kila kitu kitakuwa wazi kama ni kweli tumemsajili Feisal pamoja na wachezaji wengine tunaohusishwa nao.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live