Wachezaji 24 wametajwa katika safari ya Simba SC kuelekea nchini Uganda tayari kwa mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Vipers SC.
Simba SC itaondoka jijini Dar es salaam leo Alhamisi (Februari 23) majira ya jioni kuelekea Uganda, ambako utapigwa mchezo huo utakaokuwa na umuhimu mkubwa kwa Miamba hiyo ya Msimbazi.
Kupitia Kurasa za Mitandao ya Kijamii ya Simba SC, Orodha ya Wachezaji wanaosafiri imeonekana.
Orodha ya wachezaji wa Simba SC wanaosafiri kuelekea Uganda kwa ajili ya mchezo dhidi ya Vipers SC.
Wakati huo huo Meneja wa Habari na Mawasilino Ahmed Ally ameendelea kuwahimiza Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kuendelea kuwa wamoja, na kuepuka mikumbo ambayo imedhamiria kuwaondoa kwenye malengo ya ushindi.
Ahmed Ally ametumia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuwasisitiza Mashabiki na Wanachama kuwa kitu kimoja, huku akiendelea kusisitiza Mchezo Dhidi ya Vipers SC ni muhumu kutokana na timu yao kuhitaji matokeo.
Ahmed Ally Ameandika: Kikosi chetu kinataraji kuondoka leo jioni kuelekea Uganda kuwafuata Vipers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika Jumamosi hii.
Huu ni mchezo muhimu kwetu, ambao utatoa taswira yetu ya ushiriki wa ligi ya mabingwa msimu huu. Mechi hii inatuhitaji sana na Wana Simba kuunganisha nguvu ili kufanya vizuri.
Hatuna option zaidi ya kushikamana na kupambana kila idara ili tupate matokeo yatakayofufua matumaini yetu.
Njia pekee ya kufanikiwa kwenye nyakati ngumu ni kuwa wamoja na kufocus mbele
Inawezekana kabisa kuchukua points 3 Uganda lets goo Wana Simba?.
Kauli hii ya Ahmed inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Simba kupoteza mchezo wao dhidi ya Horona na ule wa Raja Casablanca katika dimba la Mkapa.