Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katwila wasikie wanao huku!

Mtibwa Sugar Zuberi Katwila Signs For Ihefu Fc 1bwhtnuvf7id61rxykq5oiz5ho Katwila wasikie wanao huku!

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By OLIPA ASSA BAADHI ya wachezaji wa Mtibwa Sugar, wamefunguka namna walivyokuwa wanaishi na kocha Zuber Katwila aliyetimkia Ihefu, kwamba alikuwa baba, kaka, rafiki na mshauri kwao nje ya uwanja.

Katwila ameachana na Mtibwa ikiwa imecheza mechi sita, ikishinda moja, sare mbili na vipigo vitatu, huku aliyeachiwa mikoba yake, Vicent Barnabas akianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo katika mchezo wake wa kwanza.

Winga wa timu hiyo, Haruna Chanongo alisema kuondoka kwa Katwila ni sawa na baba kuondoka nyumbani, ambapo siku za mwanzo lazima vipo vitu ambavyo vitayumba mambo mengine yakiendelea kuwekwa sawa.

“Nimetolewa mfano wa baba akiondoka nyumbani, lazima kuna vitu ambavyo vitayumba kwa muda huo, ingawa lazima kadri siku zinavyokwenda kila kitu kinakaa mahala pake, ingawa najisemea binafsi sio mchezaji mwingine,” alisema Chanongo,

Aliongeza: “Akiwa kwenye majukumu yake ni kocha ambaye alikuwa hana mchezo na kazi, neno lake kubwa alilokuwa anasema tuone fursa zilizopo kwenye soka, ambazo zitatokana na kujituma kwetu, nje ya hapo alikuwa baba, kaka na rafiki, kuhakikisha hatuharibikiwi,” alisema.

Naye beki wa timu hiyo, Dickson Job alisema kwakuwa kazi ya soka kambi ni popote atajitahidi kuyafanyia kazi yale ambayo kocha Katwila alikuwa akiwaelekeza na kwamba anamtakia majukumu mema kwenye maisha yake mapya.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz