Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katwila mali ya Mtibwa Sugar, kutambulishwa muda wowote

Katwila Kocha Zuberi Katwila

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya tetesi za siku kadhaa kumhusisha Kocha Zuberi Katwila kutua Mtibwa Sugar, kocha huyo muda wowote kuanzia leo atatangazwa rasmi na wakata miwa hao wa mkoani Morogoro.

Mtibwa Sugar kwa sasa haina kocha mkuu baada ya kuachana na Habibu Kondo kutokana na timu hiyo kupata matokeo yasiyoridhisha hivyo imebaki na kocha msaidizi, Awadh Juma.

Hata hivyo timu hiyo kongwe nchini iliyowahi kutwaa ubingwa miaka miwili mfululizo 1999 na 2000 msimu huu haijawa na matokeo mazuri ikiwa nafasi ya 15 kwa pointi mbili, ikicheza mechi sita.

Katwila aliyewahi kuichezea timu hiyo miaka ya nyuma, kwa sasa hakuwa na timu baada ya kuachana na Ihefu waliofikia makubaliano ya kimkataba kuachana takribani wiki mbili zilizopita.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amethibitisha hilo akisema muda wowote watamtamburisha kocha huyo.

"Ni suala la muda tu hata leo anaweza kuwa kwenye uzi wa Mtibwa Sugar, tunajua kwa sasa hatuna kocha mkuu hivyo Katwila ni mtu sahihi sana kwetu kwani tunamfahamu na anatufahamu," amesema Kifaru.

Kwa upande wa Katwila amesema bado hajasaini japokuwa lolote linawezekana kuanzia leo kumwaga wino kuinoa timu hiyo aliyowahi kuichezea na kuifundisha.

"Bado sijafika ila ndio uelekeo, nadhani nikikamilisha tutaweza kuzungumza zaidi, kule ni nyumbani hakuna ugeni wowote" amesema Katwila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live