Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katwila kufanya maamuzi magumu

Zuberi Katwila Mtibwa.png Katwila kufanya maamuzi magumu

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema atalazimika kufanya uamuzi mgumu wa kupunguza wachezaji kikosini kwake dirisha hili dogo lililowazi hadi Januari 15, 2024, ili kusajili mashine mpya.

Hiyo ni kutokana usajili wa wachezaji wote 30, wanaotakiwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF), katika timu za Ligi Kuu.

Akizungumza na gazeti hili, Katwila aliweka wazi jambo hilo huku akisisitiza lazima uamuzi mgumu ufanyike ili kusajili wachezaji wapya.

“Kabla ya kusajili wachezaji wapya tunahitaji kupunguza waliopo, ni uamuzi mgumu lakini lazima ufanyike ili mambo mengine yaendelee.

“Wapo tutakaowatoa kwa mkopo na wengine tutaachana nao ili kuleta wengine watakaoongeza nguvu kwa watakaobaki lengo ni kuinusuru timu kutoka huku iliko,” alisema Katwila aliyewahi kuwa mchezaji wa timu hiyo.

Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Bara msimu wa 1999 na 2000 kwa sasa wapo mkiani mwa msimamo wenye timu 16 wakikusanya pointi tano tu katika mechi 13, wakiwa wameshinda mchezo mmoja pekee, sare mbili na kupoteza 10 na kuruhusu nyavu zao kuguswa mara 28 na kufunga mabao 12.

Leo watakuwa uwanjani kucheza mechi ya 14 ya Ligi Kuu dhidi ya Mashujaa, mechi itakayopigwa kuanzia saa 10:00 jioni, Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live