Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katwila alimwa faini kwa kuchelewesha watoa huduma ya kwanza

Zubery Katwila Katwila alimwa faini kwa kuchelewesha watoa huduma ya kwanza

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zuberi Katwila ametozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kuonekana akiwashawishi maofisa wa huduma ya kwanza, kuchelewa kwa makusudi kuingia uwanjani kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.

Katwila anadaiwa kufanya hivyo wakati akiwa Kocha wa timu ya Ihefu ambapo timu hiyo ilikuwa ikicheza na Yanga katika uwanja wa Highland Estate, jijini Mbeya.

Wakati tukio hilo linafanyika, Ihefu ilikuwa mbele kwa mabao mawili dhidi ya wapinzani wao Yanga, iliyokuwa na bao moja.

Taarifa ya Bodi Ligi Kuu iliyotolewa leo Alhamisi Oktoba 19 na kusambazwa kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa "bodi imetafsiri kitendo hicho kama kupoteza muda.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live