Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katwila: Ihefu ni namba

Zubery Katwila Kocha Msaidizi wa Ihefu, Zuberi Katwila

Sat, 6 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Ihefu ikikosa mchezaji kwenye mbio za kuwania ufungaji bora ligi kuu hadi sasa, benchi la ufundi limesema tatizo ni ufinyu wa namba, huku likikiri ugumu wa kupata kikosi cha kwanza.

Ihefu licha ya mwenendo mzuri ilionao kwenye ligi kuu kwa sasa, lakini haina mchezaji aliye kwenye vita ya ufungaji bora ambapo kinara wao wa mabao, Raphael Daudi ‘Loth’ ametupia matano tu, huku Jafar Kibaya akiwa na manne.

Kwa sasa staa wa Yanga, Fiston Mayele ndiye kinara wa mabao akiwa amefunga 16, huku Moses Phiri na Saido Ntibazonkiza (Simba) wakifuata kwa mabao 10 kila mmoja.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Zuber Katwila alisema kukosekana kwa wachezaji wao kwenye orodha ya wafungaji vinara ligi kuu ni kutokana na ufinyu wa namba kwani hakuna mwenye uhakika wa kucheza dakika 90.

Alisema mbali na vita ya nafasi kikosini hata benchi la ufundi hukuna sana kichwa kuamua nani aanze au kusbiri benchi kutokana na kila mmoja kuwa na uwezo binafsi.

“Kwanza tulikuwa na mkakati wa kuipambania timu kutafuta matokeo, kwa hiyo unakuta hakuna mwenye uhakika wa namba kwa sababu kila anayecheza anaweza asimalize dakika 90,”

“Hata benchi la ufundi tunatumia nguvu na akili nyingi kupata kikosi cha kwanza, mfano sehemu ya mbele tuna mastaa nane utamuanzisha nani na umuache yupi benchi,” alihoji Katwila.

Kuhusu kupoteza mechi tatu mfululizo ikiwamo moja ya Kombe la Shirikisho (ASFC), Katwila alisema matokeo ya mpira licha yao kuamini watashinda zote na kwamba kwa sasa wanajiandaa kutopoteza tena kati ya zilizobaki.

“Lengo ilikuwa ni kushinda mechi zote lakini mpira una matokeo yake na sasa tunaendelea kujipanga na michezo mitatu iliyobaki kumaliza nafasi nzuri,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti