Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katumbi yamkuta mapya DR Congo

Moise Katumbi Kumenyana Na Tshisekedi Uchaguzi Mkuu 2023 DRC Katumbi yamkuta mapya DR Congo

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Tajiri wa timu ya TP Mazembe, Moise Katumbi yamemkuta mapya baada ya kuzuiwa kusafiri kwenda kutazama dabi ya watani kati ya timu yake na FC Lupopo inayopigwa leo.

Muda mfupi ujao Mazembe itashuka uwanjani kumenyana na Lupopo mechi itakayochezwa Jiji la Kalemie ukihamishwa kutoka Jiji la Lubumbashi ikihofiwa mchezo huo kuweza kuleta ghasia kubwa kutokana na upinzani wa timu zote mbili.

Katumbi ambaye ni mmoja wa wagombea wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo amefika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Lubumbashi maarufu kwa Luano tayari kwa safari na kukutana na zuio hilo.

Bilionea huyo amekutana na taarifa ya mamlaka ya anga kuwa ndege yake binafsi imekosa kibali cha kutua Jiji la Kalemie hatua ambayo itamfanya kuikosa mechi hiyo.

Inaelezwa mbali na kuhofia machafuko ya vurugu zinazoweza kutokea baina ya mashabiki wa klabu hizo mbili kulikuwa na kila dalili za Katumbi kuzuiwa kwenda Jiji la Kalemie kutokana na mgombea huyo kuanza kulalamikia mchakato wa uchaguzi huo unasubiriwa kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.

Mapema wiki hii Katumbi amesikika akikosoa mchakato wa uchaguzi wa nchi hiyo akidai mambo mengi hatakwenda kwa usafi katika kuondoa udanganyifu wa matokeo hayo ambayo mpaka Sasa mpinzani wake mkubwa rais Felix Tshekedi anayeongoza kwa mbali

Chanzo: Mwanaspoti