Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katumbi: Mazembe tunakwenda kuulinda ushindi Tunisia

Katumbi Mazembe . Moise Katumbi na TP Mazembe

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tajiri wa TP Mazembe Moise Katumbi amesema licha ya ushindi mwembamba ambao timu yake imeupata watakwenda kuulinda ili wafuzu hatua ya nusu fainali ya Mashindano ya African Football league.

Mazembe ikiutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kama Uwanja wao wa nyumbani jana wameshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Esperance Sportive de Tunis, na Sasa timu hizo zitarudiana wiki ijayo.

Katumbi amesema ingawa hesabu zao zilikuwa kupata ushindi mkubwa lakini wanayachukua matokeo hayo kwa mlengo chanya tayari kwa mechi ya marudiano.

"Bado tunajenga timu yetu, jambo zuri timu imeshinda hii ni sawa na kusema tumemaliza dakika 45 za kwanza tutakwenda kumalizia zingine kule kwao Tunisia.

"Tutakwenda kuulinda ushindi huu au kuutanua zaidi tulitaka sana ushindi mkubwa lakini haukupatikana, nimefurahi kuona Watanzania wametupa nguvu sana kwa kutushangilia tunawashukuru sana wamekuja wengi sana.

Bilionea huyo ameongeza kuwa timu yao itaondoka kesho kuwafuata Esperance kwa ndege maalum ya kukodi itakayopunguza uchovu wa safari kwa wachezaji wake endapo wangetumia ndege ya biashara.

"Wakati huu serikali yetu ya Congo haitusaidii sana tumelazimika kukodi ndege itakayosafirisha timu pekee itaondoka kesho ili wawahi kupumzika, tumeona tutumie njia hii ili safari iwe fupi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live