Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katika Dunia ya Achraf Hakimi mapenzi ni Biashara

Ashraf Hakimi X Uarabuni Achraf Hakimi

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: Tanzaniawe

Mapenzi ni biashara nyingine mpya ambayo bidhaa ni wewe au mimi,kadiri unavyopata fedha na umaarufu kuna kundi kubwa la wanawake wanavutiwa kuinunua hiyo bidhaa ili siku za usoni iwe faida.

Mama zetu hawana imani kabisa na wapenzi wetu kwasababu mwanamke ndio kiumbe anayemjua mwanamke vizuri linapokuja suala la vita ya mali.Mama zetu wanajua kabisa sisi ni bidhaa inayosubiriwa kuuza siku za karibuni.

Wanaume masikini hawawezi kuwa bidhaa muhimu kwasababu wanawake wa siku hizi wanafahamu baada ya mapenzi kwenda kushoto makaratasi ya benki yatakuwa hayana mate ya kutosha.Mapenzi yameondoka kwenye mapenzi yamegeuka mchezo wa kuiba fedha.

Ameandika Omar Kombo

Chanzo: Tanzaniawe