Taarifa za ndani zinadai Manchester City na West Ham zilishafikia makubaliano ya kuuziana Lucas Paqueta kwa ada ya uhamisho ya Pauni 85 milioni kabla ya dili hilo kusimama kutokana na tuhuma za kubeti zinazomkabili fundi huyo wa kimataifa wa Brazil.
Taarifa za ndani zinadai Manchester City na West Ham zilishafikia makubaliano ya kuuziana Lucas Paqueta kwa ada ya uhamisho ya Pauni 85 milioni kabla ya dili hilo kusimama kutokana na tuhuma za kubeti zinazomkabili fundi huyo wa kimataifa wa Brazil. Awali West Ham ilihitaji Pauni 95 milioni ili kumuuza staa huyu lakini baada ya majadiliano ikakubali kushusha bei na wakati wowote dili hilo linaweza kusambaratika kutokana na kiungo huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 kuchunguzwa kwa ukiukaji wa kanuni za kamari.