Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaseke awatonya Mbeya City

Kaseke Pic Kaseke awatonya Mbeya City

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiraka wa Singida Big Stars, Deus Kaseke ametoa ya moyoni. Ameipa mbinu timu yake ya zamani ya Mbeya City kama inataka kurejea kwenye makali yake ni kuhakikisha wanaenda na spidi ya soka la sasa.

Kaseke alitokea katika klabu hiyo ambayo ilimtambulisha kwenye Ligi Kuu msimu wa 2012/2013.

Kiraka huyu alipoenda mwaka huo alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao waliipandisha timu hiyo kutoka Ligi Daraja la kwanza hadi Ligi Kuu kisha na kuwa miongoni mwa timu tishio ikimaliza miongoni mwa timu nne za juu.

Kwa sasa timu hiyo haijawa tishio kama zamani na ndipo Kaseke alisema kwa ufupi aina ya wachezaji ambao walikuwepo siku za nyuma wakati timu hiyo inapanda Daraja ni tofauti na sasa.

“Mpira unabadilika sana ni tofauti na miaka ya nyuma, kwahiyo kile ambacho umefundisha siku za nyuma kinakuwa tofauti na sasa hivyo lazima ubadilike;

“Wakati huo huo siku zinavyozidi kwenda watoto wanabadilika, vyakula na vitu vingine kwahiyo ni ngumu kupata watu wale wa miaka ya nyuma ambayo timu hiyo ilikuwa tishio,”alisema Kaseke.

Kaseke alidumu kwa misimu miwili katika timu hiyo na alipoonyesha uwezo wake aliziingiza vitani timu za Simba na Yanga lakini baadae aliamua kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa miaka miwili. Unakubaliana na maoni yake, tupe mtazamo wako.

Chanzo: Mwanaspoti