Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaseke, Kalolanya kurejesha tabasamu

Kakolanya Yt.jpeg Beno Kakolanya

Sun, 9 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wadau na mashabiki wa soka jijini Mbeya wameombwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa hisani utakaowakutanisha wachezaji wa ligi kuu na kombaini ya Mkoa wa Mbeya utakaopigwa Jumamosi katika uwanja wa Sokoine.

Akizungumza winga wa Singida Fountain Gate, Deus Kaseke alisema katika kugusa maisha ya wasio jiweza wameamua kuandaa mechi hiyo maalumu kwa lengo la kutafuta fedha ili kuwasaidia.

Alisema japokuwa siyo mara ya kwanza kuandaa tukio hilo, ambapo mwaka huu wameamua kuandaa mechi hiyo kesho Jumamosi, ambapo wachezaji mbalimbali wa ligi kuu watachuana dhidi ya Mbeya Kombaini.

“Zaidi tuwaombe wadau na mashabiki waje kwa wingi kutusapoti, lengo kubwa ni kuona tunafanikisha kuwagusa wasiojiweza kama wagonjwa, yatima na waishio maisha magumu, sisi wachezaji tumejipanga,” alisema nyota huyo wa zamani wa Mbeya City na Yanga.

Aliongeza kuwa nia ya wachezaji ni kuona furaha na amani ikitawala kwenye jamii na kwamba wao kama wazaliwa mkoani humo kiu yao ni kuwapa tabasamu jamii inayowazunguka. Mratibu wa mechi hiyo, Richard Mwakalinga alisema katika mchezo huo takribani wachezaji 10 wa ligi kuu watakuwapo akiwamo Kaseke, Beno Kakolanya, Ibrahim Ndunguli, Kenny Ally, Andrew Simchimba na Geofrey Manyasi.

Alisema kutokana na wahitaji kuwa wengi bado hawajaainisha kiasi rasmi wanachohitaji, lakini mahudhurio ya wadau na mashabiki pamoja na sapoti ya watu binafsi ndio itatoa picha kujua wangapi watafikiwa.

“Wenye uhitaji ni wengi, hivyo kuainisha kiasi bado ila tukipata hata zaidi ya Sh 10 milioni itaweza kugusa idadi kubwa, huu ni utamaduni ambao unaweza kurejesha furaha kwa jamii na wachezaji husika wote wamethibitisha,” alisema Mwakalinga.

Chanzo: Mwanaspoti