Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karim Benzema na rekodi zake Madrid

Fra Karim Bemzema

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid, Karim Bemzema alifunga mabao mawili wakati Loss Blancos ikiinyuka Shaktar Donetsk bao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ulaya na kuandikisha rekodi yake mpya klabuni hapo.

Benzema amefunga mabao hayo mawili akiwa na umri wa miaka 33 na siku 319 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid mwenye umri mkubwa kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa tangu alipofanya hivyo Ferenc Puskas ambaye alifunga mabao 4 kwenye mchezo dhidi ya Feynoord September 1965 akiwa na umri wa miaka 38 na siku 173.

Ushindi huo unaifanya Real Madrid kuongoza kundi D wakiwa na alama 9 wakifuatiwa na Inter Milan yenye alama 7 ambao jana waliinyuka Sheriff bao 3-1 , huku Shakhtar wao wanaendelea kuburuza mkia wakiwa na alama 1 pekee katika mechi 4 walizocheza.

Bao la kwanza la Bemzema lilikua ni bao la 1000 katika michuano ya Ulaya kwa Real Madrid.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live