Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karim Benzema aongeza Mkataba Mpya

Skysports Karim Benzema Real 5484694 Karim Benzema

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema imeripotiwa amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Real Madrid mpaka mwaka 2024.

Kupitia kocha wa klabu ya Real Madrid ambaye amethibitisha kua Karim Benzema ataendelea kua sehemu ya kikosi cha mabingwa hao watetezi msimu ujao akizungumza na wanahabari Ancelotti alisema ” Karim ataendelea kua namba 9 wetu kwa msimu mwingine tena na kuendelea kufanya mambo makubwa kama kawaida”

Mshambuliaji huyo alikua anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu lakini taarifa zinasema mchezaji huyo ataendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwisho wa msimu wa 2023/24 ambapo mkataba wake ndio utakua uamalizika tena.

Klabu ya Real Madrid imekua inawaongezea mikataba mifupi wachezaji wake ambao wamekua wanafikisha umri wa miaka 30, Hivo ndio sababu ya Benzema pia kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja kwakua mchezaji huyo ana umri wa miaka 36.

Klabu ya Real Madrid baada ya kumalizana na Benzema inaelezwa kwasasa ipo kwenye hatua za mwisho za kumuongezea mkataba mpya kiungo wake Luca Modric, Lakini pia wanamshawishi Toni Kroos ambae amepanga kustaafu wamuongeze mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kusalia klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live