Kariakoo Dabi ipo karibu ambapo kila timu kwa sasa inafanya maandalizi kupata matokeo mazuri. Kikubwa ambacho kinatakiwa ni umakini kwenye kila hatua.
Maandalizi mazuri kwa kila timu kwa sasa ni jambo ambalo linahitajika ili kupata matokeo mazuri. Mashabiki wanapenda kuona timu yao inashinda hilo lipo wazi.
Si wao tu hata wachezaji furaha yao ni kupata ushindi lakini hakuna ambaye atapata matokeo mazuri ikiwa hakutakuwa na maandalizi mazuri.
Muda ni sasa kwa kila mmoja kuwa kwenye utayari kuelekea mchezo ujao wa Yanga dhidi ya Simba ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
Matokeo yanapatikana ndani ya dakika 90 ili kila mmoja apate kile ambacho kitakuwa ni halali yake. Hakuna pointi tatu ambazo zitapatikana bila jasho kuvuja.
Kila mmoja na awe tayari kucheza kwa nidhamu na kuongeza ulinzi kwa mchezaji mwenzake uwanjani ili kupunguza kesi za wachezaji watakaokuwa nje wakipambania hali zao.
Presha haipaswi kuwa kubwa uwanjani bali mpira uchezwe kwa kufuata sheria 17 ambazo zipo. Masuala ya kuumizana bila sababu yanapaswa yawekwe kando.
Mpira sio vita bali ni ushindani ndani ya uwanja kwenye msako wa pointi tatu muhimu.Muda uliopo kwa sasa ni kufanyia kazi makosa ambayo yalikuwa kwenye timu katika mechi zilizopita.
Inawezekana kupata ushindi na inawezekana kupoteza lakini maandalizi na nidhamu ni vitu vya msingi kuelekea Kariakoo Dabi.