Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kariakoo Derby: Maxi Nzengeli awaita Wananchi wa kwa Mkapa

Maxi Mpiah Nzengeli Ms Maxi Nzengeli.

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Maxi Mpiah Nzengeli amewaita mashabiki wa timu yake kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati yao na wapinzani wao wa jadi Simba SC utakaopigwa Jumapili ijayo, Novemba 5, 2023 katika Dimba la Mkapa.

Maxi amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa Ligi dhidi ya Singida Fountain Gate FC uliopigwa Ijumaa, iliyopita katika Dimba la Mkapa na Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku mabao yote ya Yanga yakifungwa na staa huyo raia wa Congo DR.

"Limekuwa jambo jema kupata ushindi huu wa mabao mawili na alama tatu. Kwangu mimi kikubwa ni timu kwanza kisha mimi baadaye, hivyo ninafuraha kuisaidia timu yangu kupata ushindi.

"Nilitamani nifunge zaidi ya mabao mawili lakini nafasi hazikupatikana, hivyo ninashukuru Mungu kwa matokeo mazuri tuliyoyapata.

"Akili yetu sasa ni kuelekea mchezo ujao baina yetu na Simba, ninawaomba mashabiki wa Yanga wajitokeze uwanjani siku hiyo kwa ajili ya kutusapoti kwani uwepo wao ndiyo utatupa nguvu na ari zaidi ya kupambana kupata matokeo chanya," amesema Maxi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: