Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kariakoo Dabi, Yanga kuumana na Simba Chamazi

Yanga Simba Princess Kariakoo Dabi, Yanga kuumana na Simba Chamazi

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku tatu tu baada ya klabu ya Simba kupoteza 2-0 kwa watani zao Yanga kwenye dabi ya Kariakoo iliyopigwa kwenye dimba la Mkapa, kesho jioni itapigwa tena dabi ya Kariakoo kwa upande wa wanawake ambapo Yanga Princess watakuwa wenyeji wa Simba Queens kwenye dimba la Azam Complex Chamazi kwenye mchezo wa ligi kuu wanawake Tanzania bara (WPL).

Yanga waliopo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 21 wanawakaribisha Simba wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 31, Yanga wakiwa na mchezo mmoja wa akiba.

Je nani ataibuka mshindi? ni kesho saa 10 jioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live