Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia mgeni rasmi Mkutano Mkuu ARFA

Wallace Kariaaaaa.jpeg Rais wa TFF, Wallace Karia

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA) ambao utafanyika leo Jumapili.

Wajumbe 20 watashiriki katika mkutano huo, 12 ni kutoka katika vyama sita vya soka wilaya na wanane kutoka vyama vinne washirika na ARFA.

Katibu wa ARFA, Emanuel Antony amesema mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa kuanzia saa nne asubuhi ambapo tayari wajumbe wameanza kuwasili na kuthibisha kushiriki huku akiweka wazi kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa TFF, Karia.

“Mkutano huu ni sehemu ya kutekeleza matakwa ya kikatiba na lengo kubwa ni kujenga mpira wa Arusha,” amesema Antony.

Ameongeza katika mkutano huo kutakuwa na ajenda 12 ikiwamo inayotaka vyama vyote vya wilaya kuleta taarifa zake za utekelezaji, mkoa pia kuwasilisha taarifa zake pamoja na ajenda ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwezi Juni au Julai mwaka huu.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Longido (LDFA), Obedi Joseph amesema kuwa itakuwa ni mkutano wa kipekee kwani ndio wa mwisho kabla ya uchaguzi mkuu wa mkoa.

“Kikubwa natarajia kuona ni namna gani tumefanikiwa kama Arusha na wapi labda tunakwama na kipi tunatakiwa tukifanye ili kupata timu ya Ligi Kuu, hivyo kupitia mkutano huu mwanga utakuwepo,” amesema Obedi.

Amongeza wao Longido wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani mashindano ya vijana na ligi nyingine zimekuwa zikifanyika kwa wakati licha ya changamoto ya jiografia inayowakabili.

Katika mkutano huo, kila FA Wilaya itawakilishwa na wajumbe wawili ambao ni mwenyekiti na mjumbe wa mkutano mkuu ambapo wilaya hizo ni Longido, Arumeru, Arusha Mjini, Monduli, Karatu na Ngorongoro.

Vyama washirika na ARFA, Chama cha Soka la Wanawake (TWFA), Chama cha Makocha (TAFCA), Chama cha Waamuzi (FRAT) na Chama cha Madaktari wa Michezo (TASMA) nao watawakilishwa na wajumbe wawili, mwenyekiti na katibu.

Chanzo: Mwanaspoti