Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia anavyowabeba wakongwe

Rais Karia Picc Data Rais wa TFF, Walace Karia

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Katika vipaumbele 11 vya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia mojawapo ni kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau akiamini wachezaji wa zamani wanaweza kumsaidia kutimiza majukumu yake.

TFF kwa sasa kuna wachezaji wa zamani ambao wapo kwenye nyanja mbalimbali, jambo ambalo Karia alisema anatamani kuona mchango wao utakaolipeleka mbele soka.

“Katika vipengele 11 vya Karia kipo cha kufanya kazi na wadau na tayari nakifanya kwani nahitaji mchango mkubwa wa wachezaji wa zamani ambao wana kitu kwa taifa lao,” alisema Karia wakati anaingia madarakani Juni 2017.

Kauli yake iliungwa mkono na kocha wa timu ya taifa ya Ufukweni, Boniface Pawasa ambaye ana leseni B aliyesema ni wakati wa wachezaji wa zamani kujitokeza kusomea kozi mbalimbali kama za ukocha na uongozi ili kupata fursa ya kufanya kazi TFF.

Aliyekuwa kocha wa makipa wa Yanga na Stars, Manyika Peter Sr mwenye leseni B anayeisaka A, alisema anachofanya Karia kizaa matunda siku zijazo.

Baadhi ya wachezaji wa zamani ambao wapo nyanja mbalimbali za TFF ni Wilfred Kidao katibu mkuu wa TFF aliyewahi kuichezea Simba na Taifa Stars, Aron Nyanda mkurugenzi wa masoko alikipiga Yanga, Toto African na Taifa Stars; Danny Msangi mratibu wa Stars aliyecheza Polisi Iringa, Oscar Mirambo mkurugenzi wa Ufundi alichezea Pallsons ya Arusha.

Wengine ni Pawasa ni kocha wa timu ya taifa ya Ufukweni alicheza Simba na Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ meneja wa Stars (Yanga), Deo Lucas msaidizi kocha wa timu ya taifa ya Ufukweni (Yanga), Mwanamtwa Kihwelo meneja wa timu ya Ufukweni (Yanga) na Bakari Shime ni kocha wa timu ya taifa ya wanawake (Coastal Union)

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz