Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amezitaka klabu zinazoshiriki Ligi nchini kujitambua.
Bosi huyo wa soka nchini amekwenda mbali zaidi na kueleza kwamba kama klabu zitajitambua, ufanisi zaidi utaongezeka kwenye Ligi wanazoshiriki.
Karia ambaye ni mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa saba wa Bodi ya Ligi amesema Ligi sasa ni ya Bodi na klabu shiriki, hivyo wanapaswa kuisimamia ili iwe bora zaidi.
"Kila msimu tunatamani Ligi iwe bora, lakini itakuaje bora? ni wasimamizi na klabu shiriki kujitambua na kuifanya kwa ufanisi zaidi," amesema Karia
Amesema hivi sasa Ligi inasimamiwa kwa asilimia 100 na Bodi na haiko TFF.
"Japo utaratibu wa kisheria ili ijitegemee bado haujakamilika, lakini Bodi tayari imeanza kujitegemea na Ligi wanaisimamia wenyewe," amesema Karia