Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia: Tungepata hasara ya Sh210 bilioni mikataba ya muda mfupi

Karia Pic Data Karia

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kama wangekubali mikataba ya muda mfupi ya haki ya matangazo, Soka la Tanzania lingepata hasara ya zaidi ya Sh210 bilioni.

Karia ambaye muda mfupi ujao atakwenda kuidhinishwa na mkutano mkuu kwa wanaoafiki na wasioafiki kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho hilo ameuambia mkutano mkuu kwamba wamekusanya Sh225.6 bilioni kwenye mkataba wa miaka 10 wa haki ya matangazo ya televisheni.

"Tulikuwa tunapata Sh5 bilioni kwenye mkataba wa miaka mitano, sasa tumepata mkataba wa miaka 10 ambao wengine inawakera, tumeongeza thamani ya mkataba.

Kuhusu pesa ya haki ya matangazo ya redio, Karia amesema kuna watu wanahoji na kudai ni pesa kidogo, lakini hapo nyuma hata hicho kidogo hatukuwa nacho," amesema.

Ukosoaji wa mashabiki chachu ya mafanikio

Related Mafanikio ya Biashara United yatajwa uchaguzi mkuu TFF

Rais soka Zanzibar atoa neno uchaguzi TFFAkizungumzia kuhusu mashabiki wanaoikosoa TFF, Karia amesema mashabiki wa mpira wanaowakosoa ndio wanawapa chachu ya kujipanga zaidi.

Amewashukuru mashabikii hao na kusema pamoja na kwamba wamekuwa wakiwakosoa lakini ukosoaji wao ni chachu kwao kufanya vizuri.

"Mashabiki ni watu muhimu sana, japo wamekuwa wakitugonga gonga sana huko mitandaoni, lakini ukosoaji wao ndiyo chachu kwetu kufanya vizuri," amesema.

Amesema kuna maeneo amepanga kuyaboresha ambayo ni waamuzi, makocha, utawala bora na vyanzo vya mapato.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz