Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia: Sitomchukulia hatua mwamuzi yeyote

94768 Karia+pic Karia: Sitomchukulia hatua mwamuzi yeyote

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati uamuzi wa waamuzi wa soka nchini hivi sasa ukiwa gumzo, rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema hatochua hatua kwa mwamuzi yoyote kama ambavyo baadhi ya wadau wanataka.

Karia amekiri kuwepo na tatizo kwa baadhi ya waamuzi kwenye soka amekwenda mbali zaidi na kusema hiki kinachoendelea hivi sasa kuhusu waamuzi kinahitaji mjadara mpana.

Kauli ya Karia imekuja ikiwa ni siku kadhaa tangu kuibuka malalamiko mengi juu ya uamuzi wa waamuzi kwenye mechi za Ligi kuu ikiwamo ile ya Simba na Polisi, Simba na Namungo, Yanga na Coastal, Simba na Mwadui na Mtibwa na Azam.

"Nataka nipate taarifa ya tatizo ni nini kwa waamuzi wetu, binafsi kama rais wa TFF siwezi kuwachukulia hatua waamuzi, lakini kama mahali kunakohusika wakishindwa kufanya hivyo, mimi nitadili nao," alisema.

Alisema idara ya mashindano ya TFF itakutana na kamati ya waamuzi na Bodi ya Ligi ili kumaliza tatizo hilo haraka iwezekanavyo.

"Siwezi kuingilia kama ambavyo baadhi ya watu wanataka na wengine wanadiriki kusema nijiuzulu, lakini niwambie tu kwamba siwezi kujiuzulu kwa sababu ya waamuzi kuboronga, lakini pia sitomuadhibu mwamuzi yeyote, ila kama wahusika wakishindwa kuchukua hatua stahiki, nitadili nao wao," alisema.

Pia Soma

Advertisement
Alisema kamati ya waamuzi ni kamati huru na imeachwa ifanye mambo yake kwa uhuru ikiwamo kushughulikia hilo linaloendelea hivi sasa na kamati ya uendeshaji.

Mkurugenzi wa mashindano wa TFF, Salum Madadi alisema tayari wamepokea maelekezo kutoka kwa rais wa TFF ambayo yameanza kufanyiwa kazi na kuhusu adhabu ambazo zitachukuliwa na waamuzi gani watakumbana na rungu hilo bado linajadiliwa.

"Matatizo yameonekana na lazima hatua stahiki zichukuliwe, lakini ni hatua gani, siwezi kulisemea hilo," alisema Madadi.

Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi, Salum Chama alisema wajumbe wa kamati hiyo walikutana leo saa 9 Alasiri katika kikao kilichomalizika usiku kwa ajili ya kuchukua hatua kwa waamuzi ambao wameonekana kuboronga baadhi ya mechi.

Chanzo: mwananchi.co.tz