Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia: Kila aliyelipia kiingilio chake hatadhulumiwa

5079 Kariaaa Karia: Kila aliyelipia kiingilio chake hatadhulumiwa

Mon, 10 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia baada ya sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Simba dhidi ya Yanga iliyokuwa ichezwe Mei 8, 2021 amefunguka rasmi.

Karia amesema; “Kuna taarifa itatolewa, hiyo ndiyo itaeleza kila kitu juu ya mechi hiyo kusogezwa mbele hadi kuahirishwa, lakini sasa hata mimi sijui nini kilitokea.”

Kuhusu pesa za kiingilio za mashabiki, bosi huyo wa TFF alisema ziko salama na hakuna atakayedhulumiwa.

“Pesa haziko TFF, ziko Serikalini kwa kuwa zinakusanywa kwenye mfumo wa Serikali wa N Card, huko zilipo ziko kwenye mikono salama katika mfumo wa kielektroniki.

“Kila aliyelipia kiingilio chake hatadhulumiwa kwa kuwa mfumo wa N Card unarekodi,” alisema Karia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz