Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karia: Hela za FIFA hatuwezi kuzigawa nusu kwa nusu na Zanzibar

Karia Wallace Rais Rais wa TFF, Wallace Karia

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wadau wa Soka wakipiga kelele kuhusu suala la Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF kuminywa na Shirikisho la Soka Tanzania TFF na hasa kwenye masuala ya msingi ikiwemo fedha zinazotolewa na FIFA kwa ajili ya maendeleo ya Soka.

Rais wa TFF Wallace Karia ameweka wazi kwa nini Zanzibar hawapati nusu kwa nusu fedha zinazotolewa na CAF na FIFA.

Karia amesema;

Kuna watu wengine wanasema ile hela inayopatikana kutoka FIFA igawanywe nusu nusu (Bara na Zanzibar), kwanza huwezi kuigawa ile hela, kabla ya kuipata huwa tunakubaliana iende kwenye vitu gani, tangu uongozi wangu umeingia nimekuwa nikisisitiza ile hela iwe inatumika kwenye maendeleo ya mpira nchini" - rais wa TFF, Wallace Karia.

Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kuhusu ZFF kuwa inaminywa na TFF na badala ipambane kupata uanachama CAF na FIFA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live