Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karata za mwisho

Europa Pic Karata za mwisho

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Raundi ya 16 bora Ligi ya Europa imefikia patamu na leo timu zitatupa karata za mwisho kuamua itakayotinga robo fainali, ambapo Arsenal na Manchester United zitashuka uwanjani.

Arsenal ina kibarua dhidi ya Sporting Lisbon ambapo katika mchezo uliopita uliochezwa Lisbon timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2, na sasa vijana wa Mikel Arteta wanasaka ushindi katika Uwanja wa Emirates ili watinge robo fainali.

Arteta anajivunia kuwa na silaha zote akiwamo straika Gabriel Jesus aliyerejea kikosini atakayeongeza nguvu.

Jesus ambaye amerejea baada ya kupona jeraha la goti alicheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Fulham, pale Arsenal ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-0 wikiendi iliyopita.

Kwa upande wa Man United imetanguliza mguu mmoja ndani ikijihakikisha nafasi ya kutinga robo fainali kwa sababu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Old Trafford iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Real Betis ya Hispania.

Mechi zingine za raundi ya 16 zitakazochezwa leo Fenerbahche itaikaribisha Sevilla katika mechi itakayochezwa saa 20:45 usiku.

Mchezo mwingine utakuwa kati ya Feyenoord na Shakhtar Donetsk, Freiburg itamenyana dhidi ya Juventus zote zikichezwa muda sawa.

Mechi za saa tano usiku zitakuwa ni Ferencvaros dhidi ya Bayer Leverkusen, Real Sociedad dhidi ya Roma, Union St.Gilloise itakuwa nyumbani ikimenyana na Union Berlin. Droo ya mechi za robo fainali itafanyika kesho pamoja na ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chanzo: Mwanaspoti