Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe afichua kilichompa Ujasiri kupiga penati dhidi ya ASEC

Kapombe Show The Way Shomari Kapombe akiifungia Simba bao la pili kwa Mkwaju wa Penati

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa kulia wa Simba SC, Shomari Kapombe amesema aliamua kwenda kupiga penati katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya ASEC Mimosas kutokana na kufanyia sana mazoezi kila siku.

Kapombe amesema kila siku baada ya mazoezi ya kawaida kumekuwa na muda wa kupiga penati na hilo ndilo lilimpa ujasiri wa kwenda kubeba jukumu hilo.

Tangu kuanza kwa msimu Simba imekosa idadi kubwa ya penati, hivyo kitendo cha Mlinzi huyo kuchukua majukumu hayo hakikuwa cha rahisi kwa upande wake.

"Tunafanya mazoezi ya kupiga penati kila siku lakini juzi tulihitaji kushinda ile penati kwa kuwa dakika zilikuwa zimekwenda na tulihitaji ushindi nyumbani"

"Wakati nakwenda kupiga nilikuwa namuomba Mungu anisaidie nipate, lakini wakati huo huo naifikiria timu, familia yangu pamoja na mashabiki ambao walikuwa wanahitaji furaha kwa wakati ule na namshukuru Mungu nilifanikiwa" amesema Kapombe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live