Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe aanza dhidi ya Mtibwa

AC6875A9 58B4 4937 9B8E FC5A4C943C3B.jpeg Shomari Kapombe

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kukaa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeraha kwa muda beki Shomari Kapombe amerudi na leo ameanza Simba ikishuka dimbani kumenyana na Mtibwa Sugar.

Wakati huo huo kiungo mkabaji wa timu hiyo Mzamiru Yassin ambaye alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Azam FC, Simba ikikubali kichapo cha bao 1-0 kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano amerudi kikosini.

Simba ni wenyeji kwenye mchezo huo unaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wanashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo uliopita.

Wakati wawili hao wakirudi kocha Juma Mgunda ameendelea kuwatumia mabeki wa kati Joash Onyango na Henick Inonga kwenye safu yake ya ulinzi wakisaidiana na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Kapombe aliyerudi leo.

Eneo la kiungo mkabaji amewachezesha Jonas Mkude na Mzamiru mawinga ni Pape Sakho na Agastin Okra huku eneo la ushambuliaji akianza na Clatous Chama na Moses Phiri langoni ni Aishi Manula.

Benchi kuna Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Victor Akpani, Kennedy Juma, Mohammed Ouattara, Peter Banda, Nassoro Kapama, Habib Kyombo na Denis Kibu.

Kikosi cha Mtibwa kilichoanza ni Shikhalo, Frank, Issa, Ponera, Mwihambi, Kibabage, Mapinduzi, Ilanfya, Mpepo na Kanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live