Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe, Tshabalala wapigwa msasa

Kapombee Pic Data Kapombe, Tshabalala wapigwa msasa

Wed, 10 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Olipa AssaMore by this Author MABEKI wa pembeni wa Simba wanaoanza kikosi cha kwanza, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Shomary Kapombe, wamepewa mbinu za kuwadhibiti mawinga wenye mbio wa AS Vita katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, itakayopigwa Ijumaa hii, DR Congo.

Aliyekuwa beki wa timu hiyo na Taifa Stars, Boniface Pawasa alisema Tshabalala na Kapombe wanafanya kazi kubwa ya kukapa na kushambulia, lakini katika mchezo na AS Vita aliwataka kuwa wangalifu kutokana na uzoefu walionao wapinzani wao.

Pawasa alisema alicheza beki namba tano na mbili, hivyo anajua kazi ngumu waliyonayo inayotakiwa kutumia akili ya kutotoa mpenyo kwa wapinzani kuwashambulia kupitia pembeni.

“Mechi za kimataifa tofauti na za ligi ya ndani ambayo wamezoeana, zile watu wanaangalia nafasi ya mtu kufanya makosa kidogo tu, ndio maana nawashauri mabeki wa pembeni waepuke kujisahau,” alisema Pawasa na kuendelea kuwapa mbinu mabeki hao;

“Kuna wakati wanakuwa wanapandisha sana kushambulia na kushindwa kurudi kwa uharaka kukaba, jambo linaloweza likaleta madhara wakikutana na mawinga wenye mbio, hivyo wakawe waangalifu zaidi kwenye mchezo huo,” alisema.

Mbali na kuwapa mbinu mabeki wa pembeni, alisema hata wa kati wanapaswa kuelewana na viungo wakabaji kuhakikisha wanaanzia kuwakaba wapinzani wao kabla ya kufika ndani ya 18.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz