Beki la Kimataifa, Shomari Kapombe amesema wanajiandaa na michezo ya Kimataifa hususan mchezo dhidi ya Al Ahly mchezo wa African Football League (AFL).
Kapombe amesema, mechi ya mwisho dhidi ya wapinzani wao hao, Luis Miquisson, aliwafunga hivyo watahakikisha anawafunga tena kwenye mechi hiyo ya ufunguzi wa mashindano hayo makubwa zaidi Barani Afrika itakayopigwa Oktoba 20, 2023.
"Tutahakikisha tunatengeneza rekodi nzuri ambayo tayari tumeshaiweka kwao, kwenye uwanja wetu wa nyumbani hapa lazima tumchape na Miquisson aliyewahi kuwafunga kisha akaenda kwao, amrejea hivyo lazima tumpe ushirikiano awafunge tena," alisema Kapombe.
Michuano hiyo inaanza kufanyika kwa mara ya kwanza na inaanzia hatua ya Robo Fainali kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini kisha baada ya hapo itafuata hatua ya Nusu Fainali.