Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe: Kesho tutasahihisha makosa yetu kwa Yanga

Kapombe Na Tshabalala Mohamed Hussein Kapombe: Kesho tutasahihisha makosa yetu kwa Yanga

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kulia wa timu ya Simba, Shomari Kapombe amesema kuwa wamejiandaaa vizuri kwa ajili ya mchezo wao wa dabi dhidi ya watani zao yanga SC utakaopigwa kesho Aprili 20 katika Dimba la Mkapa.

Kapombe amesema kuwa malengo yao ni kushinda mchezo huo, hivyo kocha amewaelekeza mambo yote muhimu ya kufanya ili kutoka na ushindi huku akisahihisha makosa ya wachezaji wake ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara.

“Suala la mabeki kuruhusu mabao kila mechi, mwalimu amelifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi na makosa mengi ameweza kurekebisha. Hii itakuwa mechi ya kwanza kuona safu ya ulinzi itakavyokuwa imebadilika na kucheza vizuri.

“Mchezo uliopita tulipoteza kwa idadi kubwa ya mbao, lakini huu ni ukurasa mpya na ni mechi mpya ambayo ina mikakati yake.

“Mwalimu amefanya masahihisho kwenye kila idara kuanzia ulinzi, kiungo na ushambuliaji, hivyo ninaamini mechi itakuwa nzuri na yale makosa ya nyuma tutakuwa tumesahihisha, sidhani kama tutafungwa kama walivyotufunga mechi ya kwanza,” amesema Kapombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live