Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kapombe: Huyu Augustine Okrah mtu aisee!

Shomari Kapombe Hhhh Beki wa kulia wa Simba Shomari Kapombe

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha msaidizi wa Simba, Shomary Kapombe amesema uwezo alionyesha Augustine Okrah katika kambi hiyo ya timu hiyo inakwenda kuwa staa mpya ndani ya kikosi chao msimu ujao.

Kapombe alisema Okrah ndani ya muda mfupi ameonyesha uwezo wa kufunga na anajicho la kufanya hivyo kwani hata katika michezo ya kirafiki amekwenda kulionyesha hilo.

Alisema mbali ya kufunga amekuwa na uwezo mkubwa pindi mpira unapokuwa miguuni mwaka si rahisi mchezaji wa timu pinzani kuuchukua na anafanya tendo sahihi kama ni kutoa pasi au kuleta hatari kwa wapinzani.

“Kuna nyakati kwenye mazoezi tumekuwa tukishindana nimeliona hilo mabeki wa timu pinzani watakuwa na wakati mgumu kuhakikisha wanamzuia kwani bila hivyo atakwenda kuleta madhara zaidi na kuturahisishia kufanya kila mechi,” alisema Kapombe na kuongeza;

“Nilivyo muona huyu Okrah si katika mashindano ya ndani tu bali hata katika mashindano ya kimataifa anaweza kuonyesha ubora huko na anaweza kuhakikisha napo tunashindana zaidi kutokana na ubora wake,”

“Wapenzi wa Simba wanatakiwa kufahamu kama huyu Okrah atacheza katika kiwango kama alichoonyesha katik mechi za mashindano kama alichoonyesha huku maandalizi ya msimu ujao sioni kama atashindwa kuwa mchezaji hatari.

“Kuhusu kambi kiujumla tunaendelea vizuri wachezaji wote wapo fiti na tayari kwa mashindano, ambacho tunaendelea nacho wakati huu ni kupokea yale ya msingi kutoka kwa benchi la ufundi.”

Katika hatua nyingine Kapombe amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi siku ya Simba Day kwani kuna burudani kubwa watakuja kuitoa siku hiyo.

Kapombe alisema kila mchezaji aliyekuwa hapa kambini kwetu ana hamu ya kuja Tanzania kuonyesha ubora wake na kile walichokuja kukifuata huku Misri.

“Tumedhamiria kufanya vizuri kwenye mashindano yote msimu huu yale ya ndani na nje kama ambavyo malengo ya Simba yalivyo,” alisema Kapombe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live