Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanuni zaibana Newcastle United

Bruno Guimaraes And Alexander Isak Kanuni zaibana Newcastle United

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Klabu ya Newcastle United inadaiwa iko tayari kumpiga bei Kiungo wake, Bruno Guimaraes mwenye umri wa miaka 26, na Mshambuliaji Alexander Isak mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha hili ama lijalo ili kuepuka adhabu ya ukiukaji wa sheria za matumizi ya fedha.

Katika dirisha lililopita Newcastle ilikuwa moja kati ya timu iliyosajili kwa kiasi kikubwa cha pesa na kuifanya kuwa kwenye mtego wa kupata adhabu kama ile iliyokutanao nayo Everton au zaidi, iwapo itafanya tena usajili.

Hivyo, ili kuwa salama miamba hiyo ya St. James Park italazimika kuwatoa baadhi ya nyota wake na kura imewadondokea Bruno na lsak ambao huenda wakapigwa bei kwa pesa nyingi.

Guimaraes anawindwa na vigogo na Liverpool, Barcelona na PSG, mkataba wake unamruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 100 milioni.

Isak huenda akauzwa kwa zaidi ya Pauni 70 milioni na huduma yake inawindwa na klabu za Arsenal na Manchester Ciy.

Chanzo: Dar24