Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanuni yambeba Mzize mfungaji Bora Kombe la Shirikisho

Mzize Msk21 Clement Mzize.

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa JKT Tanzania, Edward Songo na Clement Mzize kutoka Yanga wamefungana idadi sawa ya mogoli kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la CRBB Bank.

Wawili hao kila mmoja amefunga mabao matano ambayo ni mengi kuliko mchezaji mwingine yeyote.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano, iwapo wachezaji wawili watafungana kwa idadi ya mabao;

Kanuni ya (13:1) kuhusu mshindi wa Tuzo ya Mfungaji Bora inaeleza, ikiwa wachezaji zaidi ya mmoja wamefungana idadi ya mabao njia ya kwanza itakayotumika wataangalia mabao yaliyofungwa kwa njia ya kawaida yatapewa alama mbili (2).

Mabao yatakayofungwa kwa njia ya penalti yatapewa alama moja (1) na ikiwa watalingana pia itatumika kanuni ya (13:2) inayoelezea mchezaji aliyecheza dakika chache atakuwa mshindi na ikitokea wakalingana pia itaangaliwa kanuni ya (13:3).

Kanuni hiyo ya (13:3) inaeleza, kama vigezo vyote vilivyowekwa vinafanana pia basi, nyota aliyefunga mabao mengi ugenini atakuwa mshindi.

Katika mashindano ya mtoano, mshindi atakuwa mchezaji ambaye timu yake imefika hatua ya juu zaidi kuliko mwingine na endapo hatua hii haitatoa mshindi kipengele cha iii vitatumika kwa mpangilio wake.

Mchezaji wa Yanga SC, Clement Mzize amefanikiwa Kuibuka Mfungaji Bora Katika Kombe la Shirikisho la CRDB 2024.

Mechi: 06

Mabao: 05

Hat Trick: 01

Klabu ya Yanga Sc imetwaa kombe la shirikisho la Benki ya CRDB kwa mara ya nne (4) baada ya kuifunga Azam FC, jumla ya penati 6-5 katika fainali iliyochezwa katika Dimba la Amaan, visiwani Zanzibar juzi Juni 2, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live