Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanuni ya muda yamkera Mikel Arteta

USATSI 13327388 168381809 Lowres 1024x688 1 1024x640 Kanuni ya muda yamkera Mikel Arteta

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta huenda alipenda ushindi mwembamba wa dhidi ya Crystal Palace juzi Jumatatu (Agosti 21), lakini anaamini kuzingatia muda kunaweza kuhitajika ili kuondoa kutofautiana kwa upotevu wa muda baada ya Takehiro Tomiyasu kukiuka sheria.

Washika Bunduki hao walishinda 1-0 kwa bao la mkwaju wa Penalti la Martin Odegaard katika kipindi cha pili.

Beki wa Japan, Tomiyasu alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Selhurst Park, baada ya kupata kadi ya pili ya njano kwa kumchezea vibaya Jordan Ayew dakika saba tu baada ya kuonywa kwa kudhaniwa kuwa anapoteza muda.

Sheria mpya ya msimu huu na miongoni mwa mabadiliko mengine, ni kuzuia upotevu wa muda, lakini Arteta anaamini kuwa muda huo haukujumuisha nafasi ya Tomiyasu.

Alipoulizwa kuhusu mabadiliko ya sheria, Mhispania huyo alijibu: “Kwangu mimi sio suala. Mwamuzi aliamua kupiga filimbi.

“Na sisi ni sambamba na hilo. Kitu pekee tunachoomba ni uthabiti. Ikiwa sivyo, tunahitaji kucheza na saa ili kuelewa ni nini kinachotakiwa na kisichotakiwa.

Arteta hakukubali alipoambiwa Tomiyasu alisubiri kwa sekunde 23 kabla ya kuonywa akijibu: “Haikuwa hivyo. Nadhani ilikuwa sekunde nane. Huenda tukalazimika kucheza na saa ya kusimamishwa. Hivi ndivyo viwango.

Licha ya kadi nyekundu, Arsenal walishinda kwa mara ya pili mfululizo msimu huu baada ya ushindi dhidi ya Nottingham Forest kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England.

Chanzo: Dar24