Ligi Kuu Tanzania msimu uliopita ilimalizika kwa sintofahamu ya hali ya juu kuhusu mshindi wa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu cha Mfungaji Bora kabla ya Shirikisho la Soka (TFF) kuwatuza wachezaji wote wawili waliolingana kwa mabao 17, Fiston Mayele na Saido Ntibazonkiza.
Binafsi naamini tuzo ya Mfugaji Bora anapaswa kupewa ‘Top Scorer’, yaani mtu aliyeutumbukiza mpira wavuni mara nyingi zaidi. Hata wakilingana 10 wote wapewe kama mwaka 2019 kwenye EPL walilingana watatu: Aubameyang, Mane na Salah, ambao licha ya kila mmoja kuwa na idadi tofauti ya asisti au penalti, lakini wote walipewa tuzo kwa sababu kila mmoja alifunga mabao 22.
Ndio maana tunasema kanuni zitungwe kiwerevu, zitolewe mapema na zifahamike wazi, yaani zisiwe siri.