Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanuni 12 mpya zapitishwa, ushirikina faini Milioni 20.

Simba Ushirikina.jpeg Kanuni 12 mpya zapitishwa, ushirikina faini Milioni 20.

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha kanuni 12 mpya kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ajili ya msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa na TFF imesema kuwa, kamati hiyo ilipitisha kanuni hizo, Agosti Mosi, baada ya kujadili na kufanyia kazi maoni ya wadau mbalimbali wa soka kwa ajili ya kanuni mpya za ligi.

Taarifa imesema kuwa kanuni zilizofanyiwa maboresho na kupitishwa katika kikao hicho ni pamoja na kanuni ya saba ya 'firts league' kuhusu nane bora, kanuni ya tisa ya ligi kuhusu uwanja, kanuni ya 17 kuhusu taratibu za mchezo, kanuni ya 31 kuhusu timu kutofika uwanjani, kanuni ya 47 kuhusu udhibiti wa klabu, kanuni ya 62 kuhusu wachezaji wa kigeni, kanuni ya 77 kuhusu makocha na kanuni ya 79 kuhusu maamuzi yasiyokatiwa rufaa.

Baadhi ya kanuni mpya ni ya ushirikina uwanjani, ambapo sasa badala ya fainli ya Sh. 500,000, mpaka Sh. Milioni Moja, sasa timu zitakazobainika kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina, zitatozwa faini ya chini kuanzia Sh. Milioni Tano hadi Milioni10, lakini kama hali hiyo ikionekana inajirudia, klabu itapigwa faini ya Sh. Milioni 20.

Kanuni nyingine ni ya ada ya usajili wa wachezaji kutoka nje ya nchi, ambapo sasa klabu zitalazimika kulipa Sh. Milioni Nane, ambapo klabu zenye wachezaji wote 12 wanaoruhiwa kikanuni, zitalazimika kujikamua Sh Milioni 96.

Pia ipo kanuni ya kuwapiga marufuku wachezaji na viongozi kujihusisha na michezo ya kubashiri, yaani 'kubeti', huku ikiwepo kanuni kwamba kila mchezo lazima wawepo wachezaji wawili kutoka timu ya vijana, ambao watakuwa wameorodheshwa kwenye orodha  ya wachezaji waliovaa jezi.

Pia ipo kanuni inayowataka makocha wote wakuu wa kigeni nje ya Afrika wawe angalau wana cheti cha ukocha cha 'Pro Diploma', na wasaidizi wa kigeni nje ya Afrika wanatakiwa kuwa na elimu ya 'Diploma A.'

Chanzo: www.tanzaniaweb.live