Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kante anukia Hispania, Barcelona kumchukua kimafia

Ngolo Kante?fit=700%2C394&ssl=1 Kiungo wa Chelsea, Ngolo Kante

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

BARCELONA ipo kwenye hatua nzuri kukamilisha usajili wa kiungo wa Chelsea N’Golo Kante, dirisha lijalo la majira baridi baada ya mazungumzo ya wawakilishi wa Kante na mabosi wa Chelsea kutofikiwa mwafaka hadi sasa.

Kante ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu kwa sasa ni majeruhi na anatarajiwa kupona mwezi ujao na hali hiyo imesababisha akose hadi Kombe la Dunia.

Barca inataka kumsajili Kante ili akawe mbadala wa staa wao, Hispania Sergio Busquets ambaye anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Licha ya kumsajili Franck Kessie dirisha lililopita la majira ya kiangazi, staa huyo ameshindwa kumshawishi kocha wao Xavi Hernandez ambaye ndio amependekeza kuwa apelekewe Kante.

Mazungumzo baina ya wawakilishi wa Kante na Chelsea yameshindwa kufikia mwafaka kwa sababu staa huyo anahitaji mshahara mnono zaidi ya ule ambao anaupata kwa sasa.

Chanzo: Mwanaspoti