Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanoute kuikosa Prison

Kanoute Hat Trick.jpeg Kanoute kuikosa Prison

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo Mkabaji wa Simba Sadio Kanute anatarajia kuukosa mchezo wa ligi kuu bara baina ya simba na Prison uliopangwa kuchezwa kesho march 6 kwenye uwanja wa Jamhuri kutokana na kuwa majeruhi.

Kiungo huyo raia wa Mali ataukosa mchezo huo wa kesho muhimu baada ya kusumbuliwa na majeraha ya nyonga aliyoyapata kwenye mchezo wa kombe la Azam (ASFC ) dhidi ya TRA walipoibuka na ushindi wa bao 6-0 huku kiungo huyo akifunga mabao matatu pekeyake yaani (Hat trick).

Akizungumza na Mwanaspoti Kocha msaidizi wa Simba Suleiman Matola amesema wachezaji wamejiandaa kupambana licha ya kumkosa kiungo huyo muhimu.

"tunatarajia kumkosa Sadio Kanute kwenye mchezo wa kesho na hilo linatokana na kwamba anaendelea kusumbuliwa na changamoto ya Nyonga, kwakua tuna wachezaji wengi ambao wanaweza kupewa maelekezo wakacheza tumejiandaa kisaikolojia "

Kumkosa mchezaji kama Sadio kwenye timu yetu ni pigo kubwa kwakua amekuwa na umuhimu wa aina yake hususan pale anapoanzishwa kikosini lakini kwa sasa tunachofikiria ni kupata matokeo" alisema

Akizungumzia mchezo wa kesho Matola amesema wataingia na tahadhari kubwa kwakua timu hiyo imebadilika kiuchezaji na hata namna wanavyopambana

"Prison kwa siku za karibuni wamekuwa na kiwango bora uwanjani jambo ambalo linatufanya tuwape heshima yao tutakapokutana lakini Simba ni timu kubwa tuingia tukiwa na sura tofauti kwakua mchezo wa kesho ni muhimu kuushinda ili tuendelee kuwa juu kwenye msimamo"

Simba imekuwa na wastani mzuri wa kupata matokeo mbele ya Prison ambapo mchezo wa mwisho timu hizo zilipokutana Simba waliibuka na ushindi wa bao 7-1 kwenye mechi iliyochezwa uwanja wa Benjamini mkapa dar.

Chanzo: Mwanaspoti