Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanoute, Jabrane kuukosa mchezo wa marudiano

Kanoute Sadio KK Kanoute, Jabrane kuukosa mchezo wa marudiano

Sun, 10 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mkabaji wa simba Sadio kanoute na nahodha wa timu ya Wydad, Yahya Jabrane wataukosa mchezo wa marejeano wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya makundi utakaochezwa Desemba 19, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kanoute na Jabrane wote wataukosa mchezo huo kwa sababu za kikanuni za kuwa na kadi tatu za njano.

Kanoute alipata kadi ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas wakati Simba akicheza nyumbani, ya pili alipata kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy pindi Simba ilipocheza ugenini na kadi ya tatu ameipata leo kwenye mchezo dhidi ya Wydad Casablanca, Simbaa ikicheza ugenini huku Jabrane yeye akipata kadi ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy, ya pili dhidi ya ASEC Mimosas na ya tatu ameipata leo dhidi ya Simba.

Hadi sasa katika msimamo wa kundi B CAFCL michezo mitatu waliyocheza namba moja ni ASEC Mimosas pointi 7, namba mbili ni Jwaneng Galaxy point 4, namba tatu ni Wydad point 3 huku simba akishika mkia akiwa na pointi 2 baada ya kupata sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live