Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kane apukutisha rekodi kibao usiku wa Ulaya

Hcdtgfvuy Kane apukutisha rekodi kibao usiku wa Ulaya

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika Harry Kane ameweka rekodi tatu tamu kabisa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika usiku ambao chama lake la Bayern Munich liliichapa Dinamo Zagreb mabao 9-2.

Kane alifikisha mabao 33 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, akivunja rekodi ya Wayne Rooney. Na sasa, hilo linamfanya Kane kuwa mshambuliaji Mwingereza aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupiga nne Allianz Arena.

Kane alivunja rekodi ya Rooney, ambaye alifunga mabao 30 kwenye mechi 85 za michuano hiyo ya Ulaya, wakati alipokuwa Manchester United. Lakini, mkali Kane, amefikisha idadi hiyo ya mabao 33 kwenye mechi 40 tu.

Ilikuwa rekodi nyingine ya Rooney ambayo Kane aliivunja kwenye kikosi cha Three Lions, Machi 2023 - na sasa amefunga mara 68 kwenye timu ya taifa, wakati Rooney ametikisa nyavu mara 53. Na usiku wa huo wa juzi, Kane aliweka rekodi nyingine ya kuwa Mwingereza wa kwanza kufunga mabao manne kwenye mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Sambamba na hilo, anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick ya penalti kwenye mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kane sasa amelingana na Fernando Morientes kwenye nafasi ya 25 ya vinara wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya - lakini akiwa juu ya Rooney, Kaka, Samuel Eto’o, Franciso Gento na staa wa Bayern, Arjen Robben ndani ya usiku huo tu mmoja.

Ligi ya Mabingwa Ulaya ilishuhudia mechi kadhaa kwa usiku wa Jumanne na Juventus iliichapa PSV ambaoa 3-1, huku Aston Villa ikishinda ugenini mabao 3-0, sawa na Liverpool iliyokuwa ugenini pia na kushinda 3-1 dhidi ya AC Milan, wakati Real Madrid iliichapa VFB Stuttgart 3-1 na Sporting CP iliilaza Lille mabao 2-0.

Chanzo: Mwanaspoti