Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kane amfikia Rooney

Hary Kane Vs Rooney Kane amfikia Rooney

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Harry Kane amekuwa mfungaji bora pacha wa muda wote wa timu ya taifa ya England akifikisha mabao 53, sawa na Wayne Rooney aliyeishikilia rekodi hiyo kwa muda mrefu, baada ya staa huyo Tottenham kufunga bao dhidi ya Ufaransa kwenye mechi ya robo fainali juzi usiku.

Kane alifunga bao kwa penalti baada ya Bukayo Saka kuchezewa rafu ndani ya boksi na kuisawazishia England iliyokuwa imetanguliwa kwa bao 1-0 la Aurelien Tchouameni.

Baadaye Olivier Giroud aliifungia Ufaransa bao la pili kwa kichwa na England ikapata penalti ya pili baada ya Mason Mount kusukumwa kwenye eneo la penalti lakini Kane akapoteza nafasi ya kuivunja rekodi ya Rooney kwa kupaisha penalti hiyo katika dakika ya 84.

Rooney alikuwa mtu wa kwanza kumsapoti Kane baada ya kuzingua kwenye mchezo huo England iking’oka na kupoteza matumaini ya kutwaa taji lake la pili tangu ilipobeba mwaka 1966.

“Nimeumizwa na matokeo yetu lakini najivunia wachezaji, walicheza kwa kujituma dakika zote, nampa hongera Kane kwa kufikia idadi ya mabao niliyofunga kimataifa, naamini atafika mbali na kunipita, sijaona mtu mwingine zaidi ya Kane,” aliandika Rooney kupitia akaunti yake ya Twitter.

Naye kiungo wa England, Jordan Henderson alimkingia kifua Kane baada ya kukosa penalti akisema: “Kane ametupigia penalti nyingi sana, amefunga mabao mengi na kutoa mchango mkubwa, England isingekuwa hapa bila ya uwepo wake.”

Chanzo: Mwanaspoti