Tottenham Hotspur baada ya kuwa na wakati mgumu kwenye mechi zilizopita, hatimaye wamefanikiwa kushinda bao 4-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa usiku wa Jumatano.
Mshambuliaji wa kimataifa wa England Harry Kane akifunga mabao mawili huku magoli mengine mawili yakitupiwa na Matt Doherty na Son Heung-min.
Pamoja na ushindi huo kuwa muhimu kwa Spurs na kocha Antonio Conte, hiyo ilikuwa mara ya kwanza wanafunga bao la kwanza la uongozi tangia Octoba 2022.
Kane, anafikisha bao 198 tangia aanze kucheza Ligi Kuu England mechi 300 zilizopita akimpita Alan Shearer mwenye bao 196.