Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kane aiota Ballon D'or

Kane Ballon D'or Harry Kane

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harry Kane anaamini kuwa Bayern Munich inaweza kumfanya kuwa mshindani mkubwa wa tuzo ya Ballon d’Or huku akijiandaaa kucheza mechi yake ya kwanza ya Bundesliga leo.

Nahodha huyo wa England yuko fiti kukabiliana na Werder Bremen katika mechi ya ufunguzi ya Bundesliga baada ya uhamisho wake wa Pauni 100 milioni kutoka Tottenham wikendi iliyopita.

Kane alisema atapata fursa ya kushinda mataji kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka ndiyo sababu kuu iliyomfanya kuhamia Bayern, lakini pia anaamini ana uwezo wa kutwaa tuzo ya mtu binafsi yenye hadhi kubwa Ulaya kama Ballon d’Or.

“Ukishinda ligi na Ligi ya Mabingwa, ni dhahiri utakuwa katika orodha ya wanaogombania tuzo hizo. Lazima kushinda vikombe vitatu ili kutimizia ndoto hizo,” alisema Kane mwenye umri wa miaka 30.

“Ninafunga mabao na tukashinda mataji kadhaa hapa, basi sitakuwa na shaka kuhusu hilo. Siku zote nasema sitaki kustaafu soka mapema na nataka kufanya mambo makubwa zaidi. Hii ndio sababu ya kuchukua uamuzi wa kujiunga na Bayern.” aliongeza Kane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live