Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe aipiga dongo Yanga "Sisi sio watu wa viporo"

Ally Kamwe Yoyote Aje Ally Kamwe.

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imewapiga dongo wapinzani wao Simba kufuatia kusogeza mbele mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ili kupata nafasi zaidi kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC mimosas ya Ivory Coast.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati akitangaza uzinduzi wa hamasa kuelekea mchezo wao wa marejeano dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria utakaopigwa Jumamosi ijayo Februari 24, 2024 katika Dimba la Mkapa na kuupa mchezo huo jina la 'Pacome Day Kitaalam Zaidi'.

Kamwe amesema kuwa, Yanga walipangwa kucheza na Polisi Tanzania katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam kesho Jumanne, hivyo mchezo huo utakuwepo kama kawaida na watautumia kwa ajili ya maandalizi kuekelea mchezo wao dhidi ya Belouizdad.

“Nguvu anazotumia mchezaji kwenye mazoezi au mchezo wa kirafiki ni tofauti kabisa na anapocheza mchezo wa kimashindano. Kwa kutambua umhimu wa ‘match fitness’, kuelekea mchezo wa Jumamosi, tulizungumza na benchi la Ufundi wakashauri tucheze mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho (ASFC).

“Kesho Jumanne, tutakuwa na mchezo wetu wa ASFC dhidi ya Polisi Tanzania pale Azam Complex. Tumeona hakuna sababu ya kudekadeka wala kujifichaficha, timu inatakiwa icheze tupate ‘match fitness’ dhidi ya CR Belouizdad.

“Nitumie fursa hii kuwaarika wanachama wa Yanga tukaribie uwanjani kuiona sumu ambayo Master Gamondi anaitengeneza kwa ajili ya Mwarabu, kule Morogoro tuliwaonyesha kidogo na kesho tunaenda kuongeza volume kidogo muone timu iko tayari kwa namna gani kuelekea mchezo wa Jumamosi.

“Viingilio kesho ni kawaida kama standard ya Azam Complex, ni Tsh 20,000 kwa VIP A, Tsh 10,000 kwa VIP B na Tsh 5,00 kwa mzunguko. Kwa hiyo mashabiki wa Yanga mje kwa wingi ili tuweke sawa ari yetu kuelekea mechi yetu dhidi ya CR Belouizdad.

“Hapa hakuna kulazalaza mechi, hakuna kulaza viporo, na kama mtu anadeka deka anataka viporo, anaona hajiamini au hana timu, sisi tupo tayari kutwanga pia na mechi zake, awaandikie Bodi ya Ligi ‘nataka Yanga waende Mwanza wakacheze mechi yangu’, tutacheza na pointi atachukua yeye," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live