Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe aanika sababu ya kutomvalisha Chama jezi ya Yanga

Chama Mwananchi 01 Kamwe aanika sababu ya kutomvalisha Chama jezi ya Yanga

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe ameendelea kujitapa juu ya usajili wa aliyekuwa kiungo wa Simba, Clatous Chota Chama.

Kamwe pia amewapongeza wachambuzi waliosifia usajili wa Chama kutoka Simba kwenda Yanga huku akioneshwa kuchukizwa na namna ambavyo baadhi ya wachambuzi wanaokejeli utambulisho wa Chama na kuwaambia kuwa huo ni mwanzo tu na watakejeli sana.

"Suala la Usajili wa Chama ni sehemu ya biashara yetu. Kila mtu anakiri kuwa usajili wa Chama ni usajili mkubwa. Najua wengi wanauliza kwanini hatujamtambulisha Chama na jezi ya Yanga.

"Mtiririko wa matukio ya usajili huu wa Chama kwetu ni fursa. Najua wengi wanatamani kujua Chama ataonekanaje na jezi ya Yanga. Hapo ndipo tunalenga kuuza usajili huu.

"Wengi wanauliza mpaka sasa tumenufaika vipi na utambulisho wa Chama. Mpaka sasa tumepokea taarifa za mashabiki wa upande wa pili ambao wamehamia Yanga akiwemo Baba Kamwe nae amemfuata Chama. Wote waliohama tunawaandalia siku maalumu ya kuwapokea," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: