Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Yanga ndiyo mabingwa rasmi wa Muungano

Hersi Yanga Gamondiz Kamwe: Yanga ndiyo mabingwa rasmi wa Muungano

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari Yanga SC, Ally Kamwe amesema Yanga rasmi ndio mabingwa wa kombe la Muungano baada ya kufanya hivyo Bara kwenye kombe la NBC premier league na kubeba kombe la FA kwa upande wa Zanzibar ambapo Fainali ndio ilipofanyika na Yanga SC kubeba Ubingwa.

“Siri ya ushindi ni kuwa na viongozi imara wanaoshirikiana na wasikivu, kuwa na wachezaji bora ambao hata kwenye nyakati ngumu wanaweza kubakia mchezoni na wakatutafutia matokeo na tatu ni kuwa na mashabiki bora ambao wanaisapoti timu yao mwanzo mpaka mwisho.

“Hii ni medali ya pili msimu huu na medali ya kwanza kutengenezwa kwenye mashindano haya. Msimu ujao msemaji mwenye medali atabakia kuwa mimi tu.

“Leo rasmi Yanga ndiyo Bingwa wa Muungano kwa sababu Yanga amechukua Ubingwa Bara akachukua na visiwani kwa hiyo ukichanganya unapata Ubingwa wa Muungano.

“Kama wazee wetu Mwl. Nyerere na Karume walivyochanganya udongo wa bara na visiwani kupata muungano ndivyo hivyo na sisi tumechanganya kombe la Bara na Zanzibar tukapata Muungano,” amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live