Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kamwe: Tumeshavuka 'level' za kuomba radhi kama Simba

Ally Kamwe Yoyote Aje Kamwe: Tumeshavuka 'level' za kuomba radhi kama Simba

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa timu yao imeshavuka level za kuomba radhi kisa matokeo mabaya ya mchezo kama ambavyo watani zao Simba SC walifanya hivi karibuni baada ya kuwa na mwendelezo wa matokeo mabovu.

Kamwe amesema hayo kupitia Sports Arena ya Wasafi FM wakati akihojiwa kufuatia sare yao dhidi ya Al Ahly.

“Tukisema tumewaacha mbali waelewe, Yanga tumevuka hata Levo za kuomba msamaha kama Makolo, tumefungwa 3-0 lakini wote mliona timu yetu ilivyocheza ila ukiwa na Timu mbovu badala uombee msamaha kwenye mechi ijayo kwa kushinda eti unaomba Msamaha kwa kujirekod”

“Tunawaambia Mashabiki wetu kesho waje kwa wingi, waje wakongwe nyoyo zao, Al Ahly anakutana na Yanga iliyoendelea iliyobadilika sana kiuchezaji chini ya Prof Gamondi,” amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live